KATIBA YA KIKUNDI CHA VIKOBA ONLINE
SEHEMU YA KWANZA
1.1 JINA LA KIKUNDI
▶Kikundi kinaitwa vikoba online.
1.2 MAKAO MAKUU YA KIKUNDI
▶Makao makuu ya kikundi hiki ni Dar es salaam ila tuna ofisi mbalimbali mikoani kama vile Arusha,Ruvuma na Mwanza..
1.3 TAFSIRI YA KIKUNDI
▶Wanachama ambao wameungana kwa pamoja kwa lengo la kupeana misaada kwa njia ya mtandao na kufanya shughuli za maendeleo ili kudumisha maendeleo ya taifa letu.
▶Kikundi kilianzishwa mwezi wa kwanza mwaka 2018.
▶idadi ya waanzilishi ni 20.
SEHEMU YA PILI
2.0 LENGO NA MAUDHUMUNI YA KIKUNDI
2.1 MADHUMUNI
i) Kuunganisha nguvu za pamoja kwa wanachama ili kujiinua kiuchumi na kujiimarisha katika masuala yote ya kimaendeleo ili kuwa na maisha bora na mazuri.
ii) Kusaidiana kwa wanachama katika shida.
iii) Kumwendeleza Mwanakikundi ili kufanikisha shughuli za ujenzi wa taiga letu.
iv) Kufanya mijadala ya kuibua shughuli za kimaendeleo miongoni mwa wanachama.
v) Katika nyanja ya uchumi wanakikundi waweze kupewa mikopo au misaada ya kuwezesha kujikimu kimaisha.
2.2 MALENGO
Kikundi kina malengo yafuatayo..
▶Kusaidiana katika shida.
▶Kuinuana kimawazo na kifikra katika kujikimu kimaisha.
▶Kuweka hisa na kukopeshana kwa wanakikundi.
SEHEMU YA TATU
3.0 UANACHAMA
3.1 Kikundi hiki kitakuwa na uanachama kama ifuatavyo..
*UANACHAMA UANZILISHI
*UANACHAMA WA KUJIUNGA
3.1.1 UANACHAMA UANZILISHI
▶Uanachama huu utahusisha wote walioanzisha kikundi,kuandika na kupitisha katiba.
3.1.2 UANACHAMA WA KUJIUNGA
▶Uanachama huu utawahusisha wote watakaojiunga baada ya kupitisha katiba ili mradi tu awe na nia njema na kikundi.
3.2 SIFA ZA UANACHAMA
▶Awe ni mzaliwa na ni mwananchi wa Tanzania.
▶Awe na akili timamu.
▶Awe mwaminifu na mwadilifu kwa vitendo na maneno.
▶Awe amekubaliana na malengo na madhumuni ya katiba hii.
▶Awe mtiifu kwa katiba,uongozi na wanachama wenzake.
3.3 KUJIUNGA NA KIKUNDI
▶Raia yeyote wa Tanzania mwenye nia ya kujiunga na kikundi anapaswa kuwasiliana na kiongozi wa umoja huu.
▶Baada ya kuomba atapewa masharti na akikidhi atapewa uanachama.
3.4 WAJIBU WA MWANAKIKUNDI
▶Kufuata Sera ya kikundi.
▶Kufuata masharti,kanuni na sheria ya kikundi.
▶Kuwashawishi wasio wanachama kujiunga na kikundi.
3.5 MIIKO YA UANACHAMA
▶Ni mwiko kutumia lugha chafu kwa wengine.
▶Ni mwiko kutumia Mali za kikundi kwa manufaa binafsi.
3.6 MATUMIZI YA MICHANGO YA KIKUNDI
▶Mwanachama ataweza kuchangiwa na kikundi endapo tu atapatwa na msiba,kuumwa ama maafa.
Kikundi kitatoa kiasi cha pesa kilichopitishwa na uanachama.
SEHEMU YA NNE
4.0 UONGOZI
Kikundi kitakuwa na viongozi wakuu ambao ni.
*Mwenyekiti
*katibu
*Mweka hazina
*Mtunza nidhamu
*Mtoa habari na msemaji wa kikundi
4.1 SIFA ZA KIONGOZI
๐Awe Anajua kusoma na kuandika.
๐Awe Mwanakikundi hai na mchapakazi.
๐Awe Mwenye busara na hekima.
๐Awe ni mtu mwenye msimamo.
๐Awe ni mtu wa Demokrasia.
4.2 HAKI ZA KIONGOZI
▶Ana haki ya kupinga uamuzi wowote wenye lengo la uonevu.
▶Ana haki ya kujitetea Mara tu akoseapo.
▶Kiongozi hataruhusiwa kupinga maamuzi halali.
4.3 VYANZO VYA MAPATO
▶Michango ya Kila wiki kwa kila mwanachama.
▶Faini zitakazotozwa kwa mwanachama.
4.4 KUBADILI KATIBA
Katiba inaweza kubadilishwa endapo kitakuwa na mapungufu au mabadiliko yeyote itakapoitajika ili mradi tu ifuate kanuni na taratibu za marekebisho.
Kwa maelezo zaidi kuhusu vikoba online piga simu no.
๐0624681545 Au
๐0743623473 "http://vikobaonline.blogspot.com"
RATIBA YA KIKUNDI YA MWAKA 2019-2020. ๐Ratiba hii inajumuisha mipango na mikakati yote ya Kikundi pamoja na vikao vya ndani na nje kwa wiki nzima kuanzia j/tatu hadi j/pili. ⭐ JUMA TATU ๐ป๐ฒ ▶Kuanzia saa 10:00am hadi saa 12:30pm Kikao cha kutathimini mapato na matumizi ya wiki nzima. ✒Kikao hicho kitaendeshwa ndani ya magroup yote ya Active members. ( kila mwanachama anatakiwa kushiriki bila kukosa). ▶Kuanzia saa 02:00pm hadi saa 06:30pm Mijadara mbalimbali inayohusu kikao na maendeleo ya Kikundi chetu. ⭐JUMA NNE ๐ป๐ฒ ▶ Kuanzia saa 10:00am hadi saa 12:30pm Muda wa kutuma matangazo mbalimbali ya biashara kwa wanachama tu. ✒muda huu ni maarumu kwajili ya matangazo ya biashara za wanakikundi na za Kikundi kwa ujumla. Huruhusiwi kujadili chochote nje ya biashara. ▶ Kuanzia saa 02:00pm hadi saa 06:30pm Muda maarumu kwajili ya kujadili chochote kinachohusu Kikundi chetu.( si lazima kuuzulia) ⭐ JUMA TANO ๐ป๐ฒ ▶ Kuanzia saa 08:00am hadi saa 10:30am...
Maoni
Chapisha Maoni